Magazeti

Stori 10 Hot Magazeti ya leo Tanzania November 12,2014

on

leot0p

MWANANCHI

Imeelezwa kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ‘VVU’ yanaweza kuongezeka nchini  hasa kwa vijana kutokana na kupungua kwa kasi ya matumizi ya mipira (Kondomu ).

Hayo yalielezwa jana na Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu DK.Florance Turuka katika mkutano wa sita  wa kutathmini maambukizi ya VVU nchini.

Alisema maambukizi mapya yameendelea kuwapo kwa sababu vijana wengi hawatumii  kondomu kujikinga.

Matumizi ya Kondomu katika jamii yamepungua na kuwafanya watu wengi hasa vijana  kupata maambukizi na Zaidi ni kutokana na mwamko mdogo kuhusu umuhimu wa kondomu kama kinga”alisema.

MWANANCHI

Askofu kiongozi wa Kanisa la Morovian Tanzania Alinikisa Cheyo amezuiwa na waumini wa kanisa hilo kuingia katika ofisi yake iliyopo Jakaranda,Mbeya kwa zaidi ya saa18.

Cheyo ambaye pia ni Askofu mkuu wa Kanisa la Morovian  Jimbo la Kusini Mgharibi alifungiwa mlango na waumini wa kanisa hilo kwa kumzuia asiingie mpaka aitishe mkutano na kumrudisha Mchungaji Nosigwa Buya ambaye alimuhamisha.

Jitihada za Askofu huyo kuwasihi waumini hao kufungua mlango huo ambao ulikua umefungwa kwa minyororo hazikufua dafu hadi alipoomba msaada kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ambaye alifika hapo na kuwaomba waumini hao kumfungulia huku akimtaka kuhakikisha anaitisha mkutano huo ili kusikiliza maoni ya waumini hao.

Akizungumza mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya Askofu Cheyo alikubali kuitisha mkutano huo ili kumaliza mgogoro huo kama kiongozi huyo wa Serikali alivyoomba.

MWANANCHI

Ilikua hekaheka iliyosababisha mitaa minne ya Tabata Jijini Dar es salam kusimama kwa saa nne baada ya kundi la vijana Zaidi ya 30 wenye nondo,mawe na visu kushambulia watu na kupora mali zao kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wanataka kulipiza kisasi.

Kundi hilo la vijana ambao mmoja wao aliuawa linafananishwa na lile la panya Road ambalo hivi karibuni lilisumbua Jiji la Dar es salaam na kuamua kufanya vurugu baada ya ugomvi kutokea baina ya makundi mawili tofauti.

Makundi yaliyodaiwa kusababisha vurugu ni la Tabata Magengeni,Kisiwani pamoja na Mtaa wa Twiga ambapo chanzo cha vurugu ni kijana mmoja kunyang’anywa simu na wenzake wa kundi jingine.

Hali hiyo iliwafanya wakazi wa maeneo hayo kusimamisha shughuli zao kwa kuhofia ugomvi huo uku wengine wakifunga maduka yao kutokana na kutanda kwa hofu ya kuvamiwa.

MWANANCHI

Mtoto Nuru Mohamed mwenye miaka 7 ameuwa kikatili na kisha mwili wake kutekelezwa kwenye nyumba ambayo haijakamilika iliyoko Majohe Kichangani Jijini Dar es salaam.

Tukio hilo ambalo lilizua hofu kubwa na huzuni lilibanika jana baada ya kupatikana kwa maiti ya mtoto huyo ambaye kabla ya mauti kumkuta alikua amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu November6.

Akisimulia tukio hilo kwa taabu huku akilia kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo,Sauda Ally alisema mwanaye alikua akicheza na wenzake nje ya nyumba yao lakini inasemekana baadaye aliondoka na babu mmoja kwa madai anakwenda nae dukani.

“Baadaye akaja mtoto wa jirani aitwaye Dula akaniambia Nuru amekwenda na babu mmoja aliyemwomba amsindikize dukani,nilinyanyuka haraka na kuanza kumwita bila mafanikio,”alisema mama huyo.

Alisema mwanaye alitafutwa bila mafaniko na ndipo asubuhi jirani yao alipopigiwa  simu kuwa kuna maiti ya mtoto imeonekana maeneo hayo huenda ikiwa ni mwanaye.

Alisema walipofika walikuta maiti ya mtoto ikiwa imefunikwa na matofali na sehemu ya kichwa ikiwa wazi huku akiwa na jeraha kubwa sehemu ya paja ndipo wakatoa taarifa kituo cha Polisi.

MTANZANIA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali itaendelea kuyalinda makabili ya Wahadzabe na Wasandawe ambayo yanategemea rasilimali Misitu kwa maisha na ustawi wao.

“Tunakua tunafanya makosa kama tunawanyang’anya rasilimali misitu makabila madogo nchini kama vile Wahadzabe na Wasandawe kwani ndiyo rasilimali pekee inayowawezesha kupata chakula cha kitosha”alisema Pinda.

Aliwataka viongozi wa Halmashauri na watu wenye uamuzi wasiwasumbue kwa kuwalazimisha kubadili maisha yao na kutoka kwenye mfumo wa Ikolojia ambao wameuzoea.

MTANZANIA

Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai amesema hali ya usalama Wilayani Kiteto ni mbaya huku silaha nyingi zikiwa zimezagaa kama ilivyo Somalia.

Ndugai alisema mauaji yanaendelea  Wilayani humo lakini Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria huku wananchi wakimwachia Mungu.

“Kiteto siyo kama Tanzania nyinyi leo mnasikia tu hamjui kitu gani kinachoendelea,hali ni mbaya sana na si mgogoro wa wakulima na wafugaji bali ni mauaji ya kutisha”alisema Ndugai.

UHURU

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe  amewataka wabunge kuacha kuleta mambo ya siasa kwenye afya ya rais Jakaya Kikwete.

Amesema Wabunge wanaokejeli Rais kwenda kutibiwa nchini Marekani ni wasiasa wanaotafuta umaarufu mbele ya jamii na kuwa wamekosa maadili.

Zitto amesema idadi kubwa ya wabunge hutibiwa nje kwa fedha za umma na wawakilishi hao kuwa na akiba ya maneno bila kujua wanakosea.

Kauli ya Zitto amekuja baada ya kejeli za baadhi ya wabunge kuhoji sababu ya rais kwenda kutibiwa Marekani baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume ambapo alifanyiwa upasuaji na sasa hali yake inaendelea vizuri.

NIPASHE

Hali ya huduma za tiba katika hospitali ya Muhimbili ni mbaya kutokana na tatizo kubwa la bajeti ya kuwawezesha wagonjwa kutibiwa kwa wakati na kupata dawa na vifaa tiba.

Kukosekana kwa fedha za kutosha za kuendesha hospitali hiyo huku ikilemewa na madeni mengi ya watoa huduma  kumefanya ubora wa huduma za kitabibu zinazotolewa kuwa duni kiasi cha mgonjwa asiye na fedha kuwa katika wakati mgumu.

Kwa muda mrefu sasa wagonjwa waliolazwa na wale wanaokuja na kuondoka wamekua wakilazimika kununua dawa kwenye maduka yaliyopo nje ya hospitali hiyo na kwingineko  kwani maduka ya hospitali dawa hazipatikani.

Imeelezwa kuwa kazi ya daktari ni kumwandia mgonjwa dawa kisha mwenyewe kwenda kununua nje ya hospitali hiyo ambapo mpaka zile dawa za maumivu kama Panadol na declofenac hazipatikani.

JAMBOLEO

Ukata wa fedha ambao umeikumba Serikali umesababisha kontena50 za dawa mbalimbali za binadamu  kuzuiliwa katika bandari ya Dar es salaam Zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Kontena hizo ambazo ni mali ya bohari kuu ya dawa MSD  zinashikiliwa bandarini kutokana na malimbikizo ya madeni  yanayofikia bilioni45 yakiwemo ya kodi na ushuru wa malipo mengine bandarini ambapo MSD haijalipa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Taarifa zinasema kiasi cha fedha ambazo MSD wanadaiwa  ni shilingi bilioni90 na kati ya hizo bilioni45 zinatokana na malimbikizo ya kutolipa ushuru kwa Zaidi ya miaka mitatu bandarini.

Kontena hizo zinazoshikiliwa  kwa kipindi cha mwezi mmoja zinatokana na ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato TRA,Kampuni ya kuhudumia mizigo TICS na mamlaka ya bandari TPA pamoja na Taasis nyingine zinazohusiana na masuala ya chakula na dawa.

JAMBOLEO

Wazazi nchini Marekani  wametiwa mbaroni  baada ya kumnywesha pombe mtoto wao wa miaka miwili huku wakijua ina madhara.

Polisi aliwataja wazazi hao kuwa ni Willium Hokson na Jasmin Moore ambao wote ni wakazi wa Atlanta waliokua wakiishia na mtoto wao.

Alisema kutokana na kumnywesha mtoto huyo kiasi kikubwa cha pombe kali alilewa chakari na  kupata madhara makubwa ikiwa kushindwa kupumua vizuri na kulegea viungo vya mwili.

Baada ya kuona hali hiyo wazazi hao walimkimbiza mtoto huyo hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kukutwa na kiasi cha ulevi wa 0.29 ambacho ni mara tatu ya kile cha kawaida.

Wazazi hao wanashikiliwa na polisi wakati uchunguzi ukiendelea na hatimaye sheria zichukue mkondo wake.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments