Michezo

Taarifa rasmi kutoka club ya Chelsea kuhusu Didier Drogba.

on

Screen Shot 2014-07-25 at 9.05.55 PMUtakua uliziona tu zile headlines za mitandao na magazeti mbalimbali duniani kuhusu uwezekano wa staa huyu wa soka Didier Drogba kurejea kuichezea Chelsea baada ya Jose Mourinho kuonyesha nia ya kumrudisha.

Sasa taarifa rasmi iliyothibitishwa na Chelsea, mzaliwa huyu wa Ivory Coast amerejea rasmi kwenye club hii kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo wakati akitia saini, Drogba amesema ‘ulikua ni uamuzi rahisi kabisa wa kuamua kufanya tena kazi na Jose Mourinho, kila mmoja anajua uhusiano wangu na hii club… imekua ni kama nyumbani’

Jose Mourinho mwenyewe amesema ‘amerudi kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora Ulaya, namjua vizuri… na amekuja kuiweka historia nyingine’

Drogba ameifungia Chelsea magoli 157 kwenye mechi 342 alizotokezea.

Screen Shot 2014-07-25 at 9.13.00 PMNi halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments