Duniani

Wachina na rekodi zao, cheki na smartphone inayokaa chaji siku 15.. (+Video)

on

Mawasiliano muhimu sana mtu wangu, ndio maana watu wengi wanaona umuhimu wa kuwa na smartphone ili mawasiliano ya njia nyingi yaweze kumfikia.

Wataalam wa mambo wakaingia kazini na kubuni kitu kinaitwa powerbank… ambayo kama smartphone yako ikiisha chaji basi hiyo inakusaidia uendelee kubaki hewani, lakini simu+powerbank ni sawa na mizigo miwili ya kubeba mkononi, usijali… Wachina wanajali mahitaji yako.

CHINA

Kwa sababu unahitaji kitu nafuu, usipitwe na stori kwamba Wachina wameingia chimbo na kuja na mzigo wa smartphone ambazo zinaweza kukaa chaji kwa siku 15, hesabu hiyo kwa lugha nyingine ni kwamba inakaa na chaji kwa wiki mbili kamili !!

Simu yenyewe inaitwa Oukitel K10000 ambayo Wachina wenyewe wamesogezewa tayari sokoni ndani ya nchi yao na pia inapatikana Marekani kwa bei ya kama dola 239 ambazo kwa TZ inasomeka kwa shilingi 515,000/=…. Kaa tayari mtu wa nguvu, mzigo unaweza kugusa sokoni Afrika pia.

Unaweza kuiangalia simu yenyewe hapa mtu wangu, kama huna imani na vitu vya kichina cheki na hiki

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments