Mix

Rais Magufuli kawapa vyeo vipya Diwani Athumani na Jaji Warioba

on

Ni habari za uteuzi mpya kutoka IKULU Dar es salaam ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amefanya uteuzi mpya kwenye sehemu sita.

  1. Rais Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera na uteuzi huu unaanza mara moja.

    Diwani Athumani

    Diwani Athumani

  2. Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) na uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.
  3. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Sylvester M. Mabumba kuwa makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanzia November 17 2016.
  4. Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la Uhandisi na usanifu Mitambo (TEMDO) na uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

  5. Rais Magufuli amemteua Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa fidia ya ardhi ambapo uteuzi wake umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

  6. Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI) na uteuzi wake umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

VIDEO: Ulizikosa dakika 16 za Rais Magufuli akitoa tathmini ya uongozi wake baada ya mwaka mmoja? bonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments