Mix

Wafungwa wawili wametoroka Gerezani Marekani, balaa wakabaki nalo wenzao.. !!

on

CNN1

Nimekutana na stori kutoka Marekani New York ambako wafungwa wawili waliohukumiwa kifungo cha maisha wametoroka jela siku chache zilizopita huku wakiwaacha AskariMagereza kwenye mshangao jinsi ambavyo Wafungwa hao wametoroka.

CNN2

Stori inasogea kutoka New York, wafungwa waliobaki  ndani yua Gereza la Clinton Correctional Facility wanalalamikia Askari Magereza kuwatesa na kuwafanyia vitendo vya kuhatarisha maisha yao kwa nia ya kuwabana ili waseme ukweli kwanini wenzao walitoroka na wameelekea wapi.

CNN3

hii ni njia ambayo wafungwa hao wawili walitumia kutoroka

Wafungwa waliobaki walikuwa wakichukuliwa mmoja mmoja na kupelekwa kwenye chumba maalum ambako walikuwa wakipigwa, wanakabwa koo, na kubamizwa ukutani na Askari ili waongee ukweli wenzao wametorokea wapi.

CNN4

wafungwa waliingizwa humu ndani, wakateswa na kupigwa.

Baadhi ya wafungwa wakaamua kupeleka mashitaka yako mbele ya Ofisa Mkuu wa Magereza, taarifa ikawafikia Serikalini na sasa hivi Askari hao wako chini ya uchunguzi.

CNN7

wale wawili waliotoroka walikuja kutokezea hapa na kuishia zao mtaani

screen-shot-2015-06-06-at-10-31-35-am

David Sweat na Richard W. Matt, wafungwa waliofanikiwa kutoroka kwenye Gereza hilo.

Hapa chini nimekusogezea kipande cha video kinachoelezea jinsi hali ilivyo huko New York.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments