Michezo

Neymar kakutwa na hatia ya ukwepaji kodi, hukumu yake je?

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar bado yupo kwenye headlines za ukwepaji kodi, kama ambavyo zilivyokuwa zinawakabili mastaa wenzake wa FC Barcelona Lionel Messi na Javier Mascherano.

Neymar ameripotiwa kukutwa na hatia ya ukwepaji kodi wa  euro milioni 56.4, kutokana na makosa mawili ya ukwepaji wakati wa uhamisho wake kutoka Santos kujiunga na FC Barcelona na mkataba wake Nike, makosa hayo yamefanyika kupitia kampuni zake za (Neymar Sport e Marketing, N & N Consultoria, N & N Administracao de Bens) kati 2012 na 2014.

150606223921-neymar-champions-league-final-super-169

Kwa mwaka 2016 pekee Neymar anakuwa mchezaji wa pili ya FC Barcelona kukutwa na kosa hilo, aliwahi kuhukumiwa mwaka mmoja  Javier Mascherano ila adhabu yake ikabadilishwa na kuwa faini. Sheria za Hispania zinaeleza kuwa mtu akikutwa na hatia ya ukwepaji kodi anaweza badili kifungo na kulipa fedha.

Kutokana na makosa hayo ya Neymar aliyoyafanya, amepewa adhabu ya kulipa faini ya euro milioni 45.9 pamoja na kulipa kiasi alichokwepa kulipa kama kodi, kwa sheria ya Hispania kama Neymar atashindwa kulipa faini hiyo, huenda akakumbana na kifungo.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments