Michezo

Neymar wa FC Barcelona kwenye headlines na gari ya milioni 600 (+Picha)

on

Hii imekuwa kawaida kwa wanasoka wengi barani Ulaya kupenda kununua magari ya kifahari kutokana na mahitaji yao lakini hii huchangiwa na mishahara yao mikubwa wanayolipwa na vilabu vyao. Mapema mwaka 2015 tuliona nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry alionesha gari lake jipya.

October 1 mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Neymar ameonesha gari lake jipya aina ya  Ferrari 458 Spider, gari ambalo thamani yake inafikia pound 200000/= ambazo ni zaidi ya milioni 600 za kitanzania. Neymar kapiga picha na gari lake hilo la kifahari na kuweka katika account yake ya instagram.

2CF8F40300000578-3256270-image-a-32_1443706780157

Neymar akiwa na gari lake jipya Ferrari 458 Spider

Neymar ambaye ni moja kati ya wachezaji walioisaidia FC Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bayer Leverkusen bila kuwa na staa tegemeo wa timu hiyo Lionel Messi, picha ya Neymar iliambatana na ujumbe huu >>>”asante mungu kwa kunipa afya na matunda ya kazi yangu kwa kutimiza ndoto yangu”

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments