Michezo

Ninayo kauli ya Neymar kuhusu yeye kutaka kuhamia Man United …

on

Kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwezi August mwaka 2015, barani Ulaya kulikuwa na stori tofauti tofauti kuhusiana na baadhi ya wachezaji nyota kuhusishwa kutaka kuvihama vilabu vyao na kujiunga na timu nyingine. Moja kati ya mastaa waliokuwa wanahusishwa kuhama timu zao ni Neymar ambaye alitajwa kuwa katika mipango ya Man United.

September 25 mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, amefunguka kuhusiana na mpango huo wa yeye kutaka kuhamia Man United katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August mwaka huu.

IwWEj

“Ni kweli tulikuwa na mazungumzo ya awali, lakini hakukuwa na nia ya dhati katika hili, awali nilisikia kuwa kulikuwa na ofa kwa ajili yangu lakini hakuna kilichofanyika kwangu”>>> Neymar

Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Man United Ed Woodward alisafiri mapema mwezi August kwenda Barcelona kwa ajili ya kukamilisha usajili wa Pedro Rodriguez kabla ya nyota huyo kujiunga na Chelsea ila Ed Woodward aliripotiwa kumjumuisha Neymar katika mipango ya Man United.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments