Top Stories

Jicho la Bill Gates laona fursa Afrika miaka 17 ijayo

on

Leo Oktoba 2, 2018 nakusogezea stori kutoka huko nchini Marekani ambapo tajiri wa pili duniani na mmiliki wa Microsoft Bill Gates kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika kuwa ifikapo mwaka 2035 Afrika ndio itakuwa ikiongoza duniani kwa kuwa na nguvu kazi kubwa hivyo kuwekeza katika elimu na afya ya vijana ndio njia sahihi ya kutumia fursa hiyo.

Inaelezwa kuwa nchi za China , India na Marekani zinatajwa kuwa na nguvu kazi kubwa duniani kwa sasa na nchi ya Tanzania inatajwa kukamata nafasi ya 27 katika orodha hiyo.

Aidha tafiti mpya inasema kuwa nchi za Tanzania , Somalia , Zambia na Angola ni miongoni mwa mataifa yatakayo kuwa na Vijana wengi zaidi duniani ifikapo mwaka 2050 na hii ina maana kwamba nguvu kazi itakuwa kubwa kutokana na wingi wa vijana.

Mkurugenzi TAKUKURU “Wakurugenzi sita Mahakamani kwa Uhujumu uchumi”

Soma na hizi

Tupia Comments