Top Stories

PICHA 8: Christopher Ole Sendeka na viongozi wengine walivyoapishwa na Rais JPM leo IKulu

on

Siku chache baada ya kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za viongozi wa serikali, leo December 10, 2016 Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

2-mtigumwe

Rais Magufuli akimuapisha Eng. Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo

3-sasabo

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye atakuwa katika upande wa (Mawasilino)

4-aloyce

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

52

Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili mara baada ya kuapishwa na Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.

5-grace_

Rais Magufuli akimuapisha Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

64

Viongozi walioapishwa wakiweka saini katika viapo vya maadili.

7

VIDEO: Hotuba ya Rais Magufuli wakati alipowaapisha Wakuu wa Mikoa kwa mara ya kwanza. Tazama hapa

Soma na hizi

Tupia Comments