Michezo

Alichosema Mrisho Ngassa kuhusu wachezaji kuhujumu timu

on

yangaMSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa, ametamka kwamba kuna baadhi ya mechi matokeo yake ni hujuma za wazi.

Ngassa amesema amekuwa akifuatilia mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara inayoendelea, lakini kuna wakati anaona wazi kuna hujuma kwa baadhi ya klabu kupanga matokeo ingawa amegoma kuzitaja mechi hizo.

Alisema kuna baadhi ya timu zimekuwa zikishindwa kuonyesha upinzani halisi ambapo wachezaji wake wamekuwa wakijirahisisha kupoteza mipira kirahisi hatimaye timu kupoteza mechi.

“Niwe wazi mimi ni mchezaji najua na nawajua wachezaji wenzangu, kuna baadhi ya timu zimekuwa zikijirahisisha kufungwa  kwa uwazi kabisa,  sisi Yanga ni wazi tumekuwa na mechi ngumu hata kama tunashinda,” alisema.

“Lakini wapo wachezaji wa timu nyingine wanaonekana wazi kabisa wanajirahisisha kufungwa kitu ambacho kitaharibu utamu wa ligi huku mwishoni.”

Source: MWANANCHI

Tupia Comments