AyoTV

VIDEO: ‘Wazee hawapati dawa mara nyingi wakienda hospitali’ -Mbunge William Ngeleja

on

Mei 11 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017

Nakukutanisha na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja  lipokuwa akichangia maoni yake….

>>>‘Ninaombi langu la muda mrefu, Wilaya ya Sengerema tuna hospitali teule ambayo inamilikiwa na watu binafsi. Leo hii hospitali ile inaweza kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uwezo wa sasa wa vitanda zaidi ya 375

Naomba kupatiwa ufafanuzi wa ruzuku katika hospitali ya Sengerema, eneo hili la huduma ya afya ni muhimu sana, tuangalie namna tunavyoweza kurekebisha bajeti zetu tukawezesha bohari za madawa kuwafikia wananchi wetu katika kufungua maduka ya madawa katika Wilaya zetu

Ombi langu ni ujenzi wa hospitali zinazomilikiwa na Serikali yenye hadhi ya Rufaa katika kanda ya ziwa, pamoja na kuwa na hospitali ya Bugando kwakweli imezidiwa. Hii ndio kanda yenye mikoa mingi zaidi lakini ina hospitali mojatu ya rufaa

Hizi huduma za wazee zinahitaji ufuatiliaji ufuatiliaji wa makini, nashukuru mmesema kutakuwa na madawati ya kutoa taarifa. Kwakweli wazee wale wakienda hospitalini hawapatiwi dawa mara nyingi. Naomba sana wazee wetu hawa tuwazingatie sana

Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii video hapa chini…

ULIIKOSA HII WIZARA YA AFYA IMEWASILISHA BAJETI YAKE YA BILIONI 845?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments