Top Stories

Ng’ombe 15 wauawa na radi mkoani Tabora

on

Radi iliyoambatana na mvua imeua ng’ombe 15 usiku wa kuamkia leo Oktoba 18, 2021, katika Kijiji cha Zaire kilichopo Kata ya Ikomwa, Manispaa ya Tabora, ambapo ndani ya Zizi kulikuwa na ng’ombe zaidi ya 30.

Serikali ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda, imefika katika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole wanafamilia.

Kufuatia hali hiyo serikali imeahidi kufanya tathmini kwa ajili ya kumshika mkono Homano Lugwesa, ambaye ni mmiliki wa ng’ombe hao.

RAIS SAMIA AANGUA KICHEKO WODINI, MTOTO APEWA JINA LA SAMIA

Soma na hizi

Tupia Comments