Usiku wa August 13 2018 zimeripotiwa taarifa za kusikitisha kuhusiana na dereva wa msanii wa muziki na mbunge kutokea Uganda Robert Kyagulagyi Ssentumu maarufu kwa jina la Bobi Wine, taarifa zilizoripotiwa kuwa dereva wa msanii huyo amepigwa risasi.
Dereva huyo ameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika mji wa Arua nchini Uganda baada ya kuuwa, mbunge wa jimbo la Kyadondo Mashariki nchini Uganda ambaye pia ni msanii Bobi Wine ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa twitter
“Polisi wamempiga risasi dereva wangu wakifikiria wamenipiga mimi, hoteli yangu kwa sasa imezunguukwa na Polisi na SFC” bado haijajulikana moja kwa moja nini kimesababisha tukio hilo.
Dereva huyo mauti yamemkuta akiwa anaendesha gari binafsi ya msanii Bobi Wine aina ya Toyota Tundra, kwa siku kadhaa zilizopita Bobi Wine alikuwa Arua katika kampeni za kumuunga mkono Kassiano Wadri.
Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”