Habari za Mastaa

Burna Boy aangukia kufanya kazi na Beyonce (+video)

on

Superstar kutokea Nigeria Burna Boy amefanya mahojiano na kipindi cha ‘The Breakfast Club’ nchini Marekani na ameweka wazi kuhusu kufanya kazi pamoja na Beyonce kwenye Album ya ‘The Lion King:The Gift” ambayo inafanya vizuri kwenye chart za Billboards.

Burna Boy alifunguka na kusema kuwa hafahamu ni jinsi gani alifikia hatua ya kufanya kazi na Beyonce ukilinganisha hakuwahi hata kukutana nae uso uso, tamko la kufanya ngoma na Beyonce lilitoka kwa mama yake mzazi ambaye ni meneja wake kutokana na yeye kutopenda mitandao ya kijamii na ‘App’ ambayo inapatikana kwenye simu yake ni ‘WhatsApp’.

Burna Boy ameweka wazi kuwa hapendi mitandao ya kijamii kutokana na watu wengi kufuatilia vitu vya watu wengine na pengine watu wangekua wanafatilia mambo yao basi Dunia ingekua kwenye sehemu nzuri na aliongezea na kusema hapendi kuongelea kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na mwanadada Stefflon Don. 

VIDEO: ‘WATARAJIE NDOA, NISHAMTAMBULISHA TUNDA KWA WAZAZI ” WHOZU

Soma na hizi

Tupia Comments