Top Stories

Mwanaume aliyefanyiwa upasuaji kupandikizwa uso Ufaransa

on

Baada ya kuishi kwa miezi miwili bila uso, mwanaume mmoja raia wa Ufaransa, Jérôme Hamon amefanyiwa upasuaji kwa mara ya pili wa kupandikizwa uso.

Inaelezwa kuwa mwaka 2010 Jerome alifanyiwa upasuaji na kupandikizwa uso na kufikia mwaka 2016 aliumwa kifua na kunywa dawa za antibiotic ambazo zilipelekea uso wake huo wa kupandikizwa kuharibika hivyo alitakiwa kufanyiwa upandikizaji wa uso mwingine.

Hadi kufikia mwezi November 2017, uso wake ulikuwa umeharibika na ilibidi wautoe na kuanza kutafuta atakaye kuwa ‘donor’ wa sura yake kwa ajili ya Jerome ili upasuaji huo ufanywe.

Kwa miezi hii yote Jerome aliishi hospitali jijini Paris, nchini Ufaransa akiwa hana uso, jambo lililofanya asiweze kusikia, kuzungumza wala kuona hadi alipopata sura mpya siku za hivi karibuni.

Jerome alifanyiwa upasuaji wa kwanza kuondolewa uso wake kutokana na kuwa na ugonjwa ambao ni wa kurithi ambao ulipelekea awe na uvimbe mkubwa usoni mwake.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya upasuaji huo Jerome ameeleza furaha yake kupata sura mpya tena ya mtu mwenye miaka 22, ikiwa yeye ana miaka 41 na jinsi upasuaji mzima ulivyokuwa wa mafanikio.

Waigizaji walivyotembelea kituo cha Rahma Orphans Iringa

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments