Michezo

Shaffih Dauda kafunguka “Katika hili natofautiana na Rais Karia”

on

Moja kati ya stori za michezo zilizochukua headlines na kushitua wengi ni post ya mchambuzi wa habari za michezo nchini Shaffih Dauda aliyoipost usiku wa March 25 na kuanza kuzua maswali.

Shaffih Dauda ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kumpinga Athumani Nyamlani kugombea nafasi ya Urais wa TFF kama mbadala wa makamu wa Rais Michael Wambura ambaye amefungiwa maisha kujihusisha na soka.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Shaffih Dauda amepost picha ya Athumani Nyamlani na kuiambatanisha na maneno haya “Sitaki kuwa mnafiki bro you don’t deserve kuwa makamu wa raisi wa TFF, katika hili natofautiana na Rais Karia,nina sababu zaidi ya milioni moja why hafai”

Kama hufahamu Athumani Nyamlani ambaye anatajwa kutaka kurudi kuwa makamu wa Rais wa TFF, aliwahi kuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo na uchaguzi uliyopita wa TFF alitangaza kugombea nafasi ya Urais kabla ya baadae kutangaza kujitoa katika mchakato huo.

EXCLUSIVE: Kingine usichokifahamu kutoka kwa Victor Wanyama wa Tottenham

 

Soma na hizi

Tupia Comments