Habari za Mastaa

Afya ya Selena Gomez sio nzuri akimbizwa hospitalini

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa muimbaji Selena Gomez anasumbuliwa na msongamano wa mawazo ambao umepelekea kumfanya afya yake kutokuwa nzuri kwa sasa.

Taarifa zinaeleza kuwa Selena Gomez alikimbizwa hospitalini wiki chache zilizopita na kupelekea kulazwa mara mbili ili kupatiwa matibabu zaidi, kwa sasa muimbaji huyo anapatiwa matibabu katika hospitali ya Cedras Sinai mjini Los Angeles Marekani.

Selena Gomez amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ‘Lupus’ pamoja na figo ambapo alifanyiwa upandikizaji wa figo nyingine mapema mwaka 2017  na inadaiwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu alikamilisha tiba ya wiki mbili mjini New York kutokana na tatizo la hofu na msongo wa mawazo.

BREAKING: Imethibitishwa MO DEWJI katekwa “wamepiga risasi juu wakakimbia nae”

Soma na hizi

Tupia Comments