Habari za Mastaa

Mwezi May Kim & Kanye West wanategemea kupata Mtoto wa nne

on

Fahamu kuwa Kim Kardashian amethibitisha kuhusu ujio wa Mtoto wake wa nne pamoja na Mume wake Kanye West kwa njia ya mama mbadala (surrogate) ambayo kupitia njia hiyo alipatikana mtoto wao wa tatu Chicago.

Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti kuwa familia ya Kim Kardashian itamtumia mama mbadala mwingine tofauti na yule ambaye aliwapatia mtoto wao wa tatu, njia hii inakuja baada ya Madaktari wa Kim Kardashian kusema kuwa Kim ana matatizo ya uzazi na pengine atapata ujauzito itakua ngumu kuzaa na ataweza kufikia hatua ya kupoteza maisha.

Mtoto huyu atakuwa wa nne kwenye familia ya West ambapo imetajwa kuwa ni wa kiume na anatarajia kuzaliwa mapema mwezi May mwaka huu 2019.

EXCLUSIVE: MAN WATER AMEJIBU HILI KUHUSU ALIKIBA NA DIAMOND

Soma na hizi

Tupia Comments