AyoTV

Ni kweli Yanga wanacheza vibaya kwa sababu hawajapewa Milioni 200 zao?

on

Afisa muhamasishaji mkuu wa Yanga SC Antonio Nugaz leo ametolea ufafanuzi kuhusiana na madai ya baadi ya mashabiki mtandaoni kuwa wachezaji wa Yanga SC kuwa wamecheza chini ya kiwango katika mechi dhidi ya KCM waliyofungwa 1-0 na mechi dhidi ya Namungo waliyotoka sare ya 1-1 kutokana na kutopewa bonas yao ya Tsh milioni 200.

Unajua Yanga kuelekea game ya Simba walioyoshinda 1-0 waliahidiwa na mdhamini wao GSM kwa mujibu wa vyombo vya habari bonus ya Tsh milioni 200 kama wataifunga Simba SC, so baada ya kucheza chini ya kiwango kwa game mbili mfululizo zilizofuatia baada ya ushindi dhidi ya Simba SC, wengi wakadai ni kutokana na kutopewa ahadi yao.

Antonio Nigaz atolea ufafanuzi nini kimekwamisha na kweli wamecheza chini ya kiwango, Nugaz aeleza sababu kubwa ya kuchelewa ni kutokana na taratibu za kibenki, kwa maana Tsh milioni 200 ni tofauti na Tsh milioni 10 ambayo kwa kawaida hutolewa kila mechi.

VIDEO: KIPIGO CHA KMC CHA WACHANGANYA YANGA “HATA SIJUI NDIO UTOPOLO WENYEWE”

Soma na hizi

Tupia Comments