Nick Cannon, ambaye ana watoto 12, alifichua kuwa anatumia karibu $200,000 kwa mwaka kwenye Disneyland, bustani maarufu ya kitalii nchini Ufaransa kwa watoto wake.
Rapa huyo na mtangazaji wa Runinga aliambia kipindi cha redio cha The Breakfast Club kwamba yeye huenda Disneyland “angalau mara moja kwa mwezi” kuadhimisha matukio maalum kama vile siku za kuzaliwa za watoto wake na kwa tafrija za likizo.
“Je! unajua ni pesa ngapi ninazotumia huko Disneyland kwa mwaka?” Aliuliza watangazaji wenzake.
“Si bure tena, na nilikuwa na watoto wawili tu wakati huo!”, Alisema kuhusu watoto wake wawili wakubwa, mapacha Morocco na Monroe wenye umri wa miaka 12, ambao ni wanawe na Mariah Carey.
“Kila siku ya kuzaliwa na Krismasi – mimi niko Disneyland angalau mara moja kwa mwezi, na kuzunguka Disney, kama, labda ninatumia $ 200,000 [shilingi milioni 502,999,924 kwa mwaka huko Disneyland,” alisema.
Alisema kuwa Disneyland ni ghali, na kuongeza kuwa gharama nyingi hukusanyika, pamoja na kulipia hoteli na mlezi.
Mnamo Septemba, alichapisha picha kwenye Instagram akiwa na watoto wake watatu katika Disneyland, ambayo alinukuu akisema ni “mahali anapopenda zaidi” na “mahali pa furaha zaidi duniani.”
Cannon ana watoto 12 na wanawake sita, tisa kati yao walizaliwa katika muda wa miaka miwili.
Hapo awali alisema hutumia zaidi ya dola milioni 3 kwa watoto wake kila mwaka.