Habari za Mastaa

Nick Minaj akataa kuchanjwa chanjo Covid-19, asema “Mtu kawa mgumba”

on

Ikulu ya Marekani imesema ipo tayari kufanya mazungumzo na Rapper Nicki Minaj ili kumuelezea kwa undani Usalama na ubora wa chanjo za corona baada ya Rapper huyo kusema anahitaji kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuamua kuchanjwa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nick alisema atachajwa baada ya kufanya utafiti wa kutosha huku akisema kwa sasa yeye atajikinga kwa kuvaa mask zenye ubora huku akiwataka na Mashabiki zake kufanya hivyo.

Nicki alisema Binadamu yangu amesema hatochanja kwasababu Rafiki yake amechanja na akapata madhara ikiwemo korodani zake kuvimba ambapo alikua akijiandaa kuoa lakini sasa Mchumba wake amesitisha ndoa. Baada ya Ikulu kumpa mwaliko wa kufanya nae mazungumzo Nicki amesema hiyo ni hatua nzuri na amekubali kwenda ———“Ikulu imenialika, nitakwenda”

Soma na hizi

Tupia Comments