Habari za Mastaa

Mambo manne ya kufahamu kutoka kwa Nicki Minaj >>> ‘Ndoa, muziki, siasa na mapenzi’ <<<..!

on

Staa wa muziki wa HipHop kutoka Marekani, Nicki Minaj maarufu pia kama The Rap Queen anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani.

minaj6

Baada ya kuchaguliwa kwenye vipengele vitatu vya The 58th Grammy Nominations, staa huyo kutoka lebo ya Cash Money Records alichukuwa time na kufanya interview na jarida kubwa la burudani Marekani, Billboard Magazine na kugusia vitu vingi ikiwemo maisha yake na Meek Mill, Siasa, Muziki, ushauri wa kimaisha  na vitu vingine kibao.

minaj4

Nicki Minaj: Billboards The No.1s Photo Shoot Cover.

Hivi ni vichache nilivyofanikiwa kuvinasa kutoka kwenye interview hiyo na Billboard Magazine:

Support anayotoa kwa Hillary Clinton:Ninamsupport Hillary kama mwanamke. Kama nimeshawishika anafaa kuwa Rais wa awamu ijayo? Bado napenda niwe na mawazo huru kuhusu kila mgombea. Bila ubishi naelewa struggle anayoipata kama mwanamke. Pia bila ubishi naelewa nafasi anayowekwa kama mwanamke akiingia sehemu ambayo imejaa wanaume zaidi- kuna wakati naamini hata yeye anaogopa, lakini pia naamini anatumia uoga huo kama silaha yake ya ushujaa. Kwa sababu kama mwanamke nimekuwa nikifanya hivyo kila mara. Kwahiyo kwa hilo ninamkubali sana“.

minaj1

Nicki Minaj: Billboard The No.1s Issue Photo Shoot.

Kuhusu mgombea mwenza wa Hillary Clinton, Donald Trump: Kuna hoja ameziongelea ambazo naamini kama asingetumia approach ya kitoto kuzifikisha mbele ya umma zilikuwa ni nzuri kwa namna yake. Lakini kwa upande wa burudani- huyu jamaa anachekesha sana. Natamani kama wangetengeneza movie ya yeye akiwa kwenye safari ya Urais. Hiyo ingekuwa reality show kubwa balaa.

minaj3

Kuhamia Los Angeles na Meek Mill:Napapenda [Los Angeles]. Nilipokuwa nahamia nilizungumza na Beyonce, kwasababu na yeye amehamia huku hivi karibuni pia. Beyonce alisema kile nilichokisema mimi mara ya kwanza nahamia huku, ambacho ni kila mmoja amekuwa mwenye furaha zaidi. Alikuwa ananiambia vitu vidogo ambavyo pengine ningeviona kama mzigo kumbe sio mzigo hata [kwa huku]. Pia aliniambia haichoshi kuamka asubuhi sana na kumpeleka Blue [mwanae] shule, kwasababu mazingira ni mazuri [na ndicho nachokiona pia].

minaj8

Pete aliyopewa Nicki Minaj na mpenzi wake Meek Mill hivi karibuni.

Je, vipi kuhusu pete aliyovalishwa na Meek Mill: Mimi na yeye hatupo-engaged. Lakini alisema angependa kunipa pete tatu kabla hajanioa. Birthday yangu inakuja, kwahiyo achangamke kunipa pete nyingine, kwasababu alishanipa moja [ya kwanza ilikuwa mwaka jana] kwenye birthday yangu iliyopita.

minaj2

Jay Z, Beyonce, Nicki Minaj & Meek Mill.

Ushauri kutoka kwa Beyonce na Jay-Z: Tuliongea nao, Jay Z na Beyonce [kuhusu ndoa]. Baada ya show yetu [Brooklyn] ya Barclays Center [ mwezi October], tulipata dinner pamoja. Walitupa ushauri mzuri sana. Nawapenda sana. Yalikuwa maongezi mazuri sana na watu tunaowapenda na kutazama kile wanachokifanya kama couple. Ile couple [Jay Z na Beyonce]  ipo mahiri sana!

minaj5

Kama atarudi kufanya mixtape zozote: Kabisa. Lazima niachie mixtape soon. Nataka niguse beats tofauti ambazo sikuzigusa hapo awali. Ningeweza kutoa single zenye beats nzito mwaka jana, lakini kwangu jambo la msingi ni kuonyesha mfano kwa marappers wengine wa kike. Kwenye game nipo juu sasa hivi na ni muhimu kuweka mfano… ni muhimu kwa wewe kuwa mkubwa kuliko muziki wako. Nina mashabiki amabao wameshajitoa kuwa na mimi maisha yangu yote kwasababu wanajua nilipoanzia. Mashabiki wanajua msoto wangu, jinsi nilivyokuwa na njaa, kwamba nilikuwa siridhiki na mafanikio madogo tu, sikukata tamaa, nilikuwa kwenye ngoma ya kila mtu na nilikuwa kikazi zaidi… mashabiki wanajua kwa hiyo ni lazima nifanye kazi kuonyesha mfano.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

 

Soma na hizi

Tupia Comments