Habari za Mastaa

Ni kweli Nicki Minaj ana ujauzito wa Meek Mill ama anatania tu?!

on

nicki_minaj1

Nicki Minaj ameweka headlines kwenye kurasa za burudani kwa siku tatu mfululizo baada ya kutangaza  kuwa ana ujauzito wa superstaa boyfriend wake Meek Mill, taarifa ambayo imewaweka mashabiki wengi roho juu baadhi wakifurahia na wengine wakiwaza kama ni kweli ana ujauzito huo.

Kwenye tour ya mji wa mwisho waliotembelea wiki iliyopita Nicki Minaj alisikika akitoa pongezi za sifa kwa Meek Mill huku akiwaomba mashabiki wampigie kelele za kutosha “baba wa mtoto wake”… so hii ishu ni kweli ana ujauzito ama anatania tu?

onika

Licha ya hayo Meek Mill ameshasikika kwenye interviews zaidi ya moja akisema kuwa anatamani sana kuwa na mtoto na Nicki lakini ikiwa tu wakiwa ndani ya ndoa. Je msimamo sasa hivi umebadilika?

Mashabiki wana maswali mengi sana, na kama wewe ni miongoni mwa mashabiki wa Nicki Minaj utakuwa umejiuliza maswali mengi sana pia juu ya hii ishu…Hapa chini nimekusogezea kipande cha video na baadhi ya tweets za Nicki za Twitter.

minaj5

 

minaj4

Nicki Minaj aka re-tweet baadhi ya tweets za mashabiki huku akicheka sana…

minaj2     minaj1

Hizi taarifa zimewaacha mashabiki wengi wakiwa haweelwi nini kina endelea kwani umepita mwezi mmoja tu toka Nicki Minaj aseme kupitia Twitter kuwa hategemei kuzaa akiwa hayuko ndani ya ndoa. Wewe unaonaje?

minaj6

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments