Habari za Mastaa

Nicki Minaj kumbe ana kipaji cha kuigiza… Haya ni mengine yakutegemea kutoka kwake!

on

Wengi tunamjua Nicki Minaj kama msanii wa HipHop mwenye hit songs nyingi kama Super Bass, Anaconda na Feeling Myself… Lakini ulishawahi kuvuta picha ya Nicki Minaj kama msanii wa kuigiza? Producer wa tamthilia je?

NICKI2

Kama wewe ni shabiki wa Nicki Minaj basi ichukue hii mtu wangu, kituo cha TV cha ABC Family cha Marekani kimetangaza kuwa rapper huyo kutoka Cash Money Records ataonekana kwenye series mpya ya comedy itakayokuwa inagusa maisha binafsi ya msanii huyo!

NICKI

Taarifa zinasema kwamba Nicki Minaj atakuwa producer wa series hiyo na pia ataonekana ndani ya series hiyo… japo inawezekana Nicki Minaj akatafuta mtu wa kuigiza kama yeye, hii ni kutokana na tweet alioipost kwenye page yake ya Twitter ikiashiria kama ataingia mtaani kutafuta vipaji vya kuigiza kwenye nafasi yake kwenye series hiyo…

NICKI2

Tutegemee vitu vizuri kutoka kwa Nicki Minaj soon mtu wangu!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments