Ufaransa imesema inasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Niger, kwa sababu viongozi wake wapya “hawataki tena kupigana dhidi ya ugaidi”.
Niger imekumbwa na ghasia za wanajihadi kwa miaka kadhaa, huku mashambulizi yakifanywa na Al-Qaida na washirika wa Islamic State.
Mshirika wa mwisho wa Ufaransa katika eneo la Sahel hadi mapinduzi, Niger inaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya usalama.
Eneo hilo limeshuhudia kuongezeka kwa ghasia, kulingana na NGO ya ACLED, huku makundi ya wanamgambo yakijaribu kuchukua fursa ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa.
Niger ilikuwa nchi ya tatu kujitoa katika mapinduzi, kufuatia Mali na Burkina Faso ambao pia walitaka Wafaransa kujiondoa.
Katika mwezi wa kwanza kufuatia mapinduzi ya Niger, kulikuwa na ongezeko la 42% la ghasia za kisiasa ikilinganishwa na mwezi uliopita.