Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la polisi nchini Nigeria, SP Abdullahi Kiyawa, inasema kuwa jeshi la polisi lilikuwa linafuatilia kilio cha wananchi kilichopokelewa na waratibu wa soko la Dansulaika GSM, Farm Centre, Kano kuhusu tukio la wizi uliotikea.
Agosti 24, watu wasiojulikana walivunja maduka kumi na moja kupitia dari za paa na kuiba baadhi ya simu za mkononi, kompyuta za mezani, Laptop na baadhi kiasi cha pesa, kadi za ATM na vifaa vingine.
Alisema operesheni endelevu iliyoongozwa na kijasusi ilianzishwa ambayo ilisababisha kukamatwa kwa Ibrahim Adamu, wa Sallari Quarters, na mtuhumiwa alikiri kwa polisi kuwa alitenda kosa hilo peke yake na kupelekea kupatikana kwa simu (106), kompyuta laptops 9.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa madai ya kesi yanayoendelea.