Mix

Alikuwa na ndoto ya kuwa staa mkubwa wa movie Nigeria, akaenda kwa mganga, kilichotokea..!?

on

Kuwa na ndoto kubwa ni kitu kizuri sana, lakini juhudi za jinsi gani tutatimiza ndoto zetu sio sawa kwa watu wote, wengine wanaamini kupiga kazi mpaka mpale juhudi za kazi zao zitakapowalipa na kuna wengine wanaoamini kuwekeza kwenye njia tofauti…

nigeria

Gloria Sule ni dada ambaye alikuwa na ndoto kubwa za kuja kuwa mwigizaji maarufu Nollywood Nigeria na alikuwa yupo tayari kufanya kitu chochote kile kutimiza ndoto zake… akiwa kwenye harakati za kutimiza ndoto hiyo Gloria alikutana na mganga Francis Kalu ambaye alimwambia kama akimpatia Naira milioni 2.1 pesa yenye thamani ya Milioni 22 kwa Tanzania basi atatimiza ndoto zake!

dreams

Gloria Sule.

Baada ya kutoa hiyo pesa, mganga huyo alimwambia ili kukamilisha dawa ya mvuto ya ustaa itambidi atimize baadhi ya masharti ya mganga huyo ikiwa kuoga nae ili kuruhusu dawa aliyompa kufanya kazi… lakini baada ya kufanya yote hayo Gloria hakuona kitu chochote kikitokea na ndipo alipoamua kwenda polisi kumshitaki mganga huyo.

dreams5

Mganga alikamatwa na kupelekwa polisi, kesi ikafika mpaka kwenye Mahakama ya Ejigbo Jijini Lagos walivyokuwa huko Francis Kalu akasema hana kesi ya kujbu kwani dada huyo alitaka mwenyewe kuchezewa… kesi hiyo imeahirishwa na imepangwa kusikilizwa tena September 21 mwezi huu.

Mganga huyo anashitakiwa kwa kosa la wizi na utapeli kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai ya Nigeria.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments