Top Stories

Uamuzi wa Rais wa Nigeria baada ya Boko Haram kuendelea kuiandama nchi yake..

on

BUHAR

Kundi la kigaidi la Boko Haram limeendelea kuua maelfu ya watu Nigeria na hivi karibuni kumetokea matukio mfululizo ya mauaji ya watu katika maeneo ya wazi.

Kufuatia matukio hayo Rais  Muhammadu Buhari, amewafuta kazi wakuu wa jeshi la angani, majini na wa nchi kavu.

buhRais huyo amewatimua maafisa hao wakuu jeshini kwa kushindwa kukabiliana na kundi la wapiganaji hao wanaoendelea kuiandamana nchi hiyo.

Buhari ambaye mwenyewe ni jenerali mstaafu aliahidi wapigakura wake katika uchaguzi mkuu uliopita kuwa atalitokomeza kabisa kundi hilo la Boko Haram ambalo ka siku 10 tu zilizopita tayari limeua watu zaidi ya 200.

Mpaka sasa bado hajazungumza mbadala wa wakuu wengine watakaochukua nafasi hizo.

Unahitaji nikutumie kila stori ninayoipata? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments