Moja ya matukio yaliyotrend au kuingia katika headlines ni pamoja na sekeseke zima la Mobahd au IMOLE kuwa Jambo la kitaifa na hii ni baada ya maelfu ya mashabiki pamoja na raia kujitokeza nchini Nigeria na kuingia barabarani kwanzia jana mpaka hii leo katika maeneo tofauti tofauti nchini humo katika harakati za kudai haki na uchunguzi wa kifo cha rapper huyo.
Waandamanaji walivaa nguo nyeusi na kubeba mabango mengi yaliyoandikwa #JusticeForMohbad.
Wajumbe wa uongozi wa Mohbad pia wakijibu kwa kusema kwamba wanathamini upendo na support kubwa iliyoonyeshwa na mashabiki na kwamba wangependa mashabiki wajiunge na maandamano ya kuwasha mishumaa na tamasha la heshima ambalo uongozi unaandaa.
Tukio hilo litafanyika Alhamisi, tarehe 21 Septemba, saa kumi na moja jioni katika ukumbi wa Lekki Phase 1 Gate na tamasha litafanyika saa mbili usiku katika Muri Okunola Park, jijini Lagos nchini Nigeria.
Mamlaka ya polisi katika Jimbo la Lagos walianzisha timu maalum ya uchunguzi mwanzoni mwa wiki hii ili kuchunguza kifo cha rapa huyo na wanatarajia timu hiyo kuwasilisha ripoti kamili ndani ya wiki mbili.
Mohbad alipata umaarufu mkubwa mnamo 2020 baada ya kuachia wimbo wake ‘Ko Por Ke’ akimshirikisha Rexxie pia ameshirikiana na wasanii wengine maarufu wa Nigeria, kama vile Lil Kesh na Davido.