Michezo

Umeona maneno ya Samuel Eto’o kuhusu Alex Song na Barcelona? yako hapa

on

1236582_10152028414426149_1018294214_nMshambuliaji wa klabu ya Chelsea na Cameroon Samuel Eto’o ameeleza kusikitishwa kwake na namna Mcameroon mwenzie Alexander Song anavyokosa nafasi ndani ya kikosi cha FC Barcelona.

Song ambae alihamia Barcelona akitokea Arsenal msimu uliopita, amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha mabingwa wa Hispania jambo ambalo linamkera Eto’o ambae anachezea Chelsea kwa sasa.

Amesema >>> ‘Song ni mchezaji anaepaswa kucheza katika timu inayompa nafasi na sio Barca, inabidi aondoke FC Barcelona manake kwa umri huu anapaswa kucheza na inabidi awe anaanza katika timu yoyote na sio tu kuwa mchezaji wa kukaa benchi.”

Umekubaliana na maneno ya Eto’o? unaonaje kiwango cha Song?

Soma na hizi

Tupia Comments