Top Stories

“Nikishinda Urais kazi siku 4, bangi ruhusa” Mgombea Kenya

on

Mgombea kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2022 kupitia Chama cha ‘Roots Party’ Profesa George Wajackoyah (62) amesema akishinda Urais atabadilisha utaratibu ili Watu wawe wanafanya kazi siku nne tu za wiki ambazo ni Jumatatu mpaka Alhamisi ili Waislamu wapate muda wa kuswali Ijumaa lakini pia atateua Mawaziri Wakuu 8 na kusimamisha katiba kwa miezi sita.

Mgombea huyu wa kiti cha Urais, Wajackoyah pia ameahidi kuhalalisha bangi iwapo atashinda kiti cha juu cha nchi.

Justina Wambui Wamae ambae ndio Mgombea mwenza akiwa pia ni Mwanamke wa kwanza kuwa mgombea mwenza wa urais katika historia ya Kenya, ameeleza kuwa anaamini biashara ya bangi itachochea uchumi unaoyumba na kuleta mapinduzi ya kina ambapo mauzo ya bangi yatasaidia pia kulipa deni la Taifa.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by CR millard ayo (@millardayo)

Soma na hizi

Tupia Comments