Top Stories

Nikk wa pili aibuka na hili “Hakuna majini yananyonya damua Kisarawe ni Ugonjwa”

on

Baada ya kuwepo taarifa za baadhi ya wananchi wanaodai kuna majini yananyonya Damu Kisarawe, Leo DC wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon a.k.a Nikk wa Pili ameibuka na kusema sio kweli bali ni Ugonjwa wa Sickle Cell ambapo wilaya yake imezindua kliniki maalum kwa ajili ya uangalizi wa watu wanaoishi na ‘Sickle Cell’ kwa malengo ya kupunguza vifo vitokanavyo na maradhi hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson Simon ameeleza kwamba kliniki hiyo itasaidia wengi kwani kwa mtu ambaye haendi kliniki akiwa na ugonjwa huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni 50% wakati yule anayeenda kliniki uwezekano wa kupoteza maisha unakuwa 7%.

PLAY KUTAZAMA VIDEO

 RAIS SAMIA MGENI RASMI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA DEMOKRASIA DUNIANI

 

Soma na hizi

Tupia Comments