Top Stories

Nikk wa pili ameeleza alivyokuwa akikesha na mtoto ili mpenzi wake asome (video+)

on

DC Nickson Simon John, maarufu kama Nikk wa Pili amezungumza baada ya mpenzi wake Joan Temu kuhitimu elimu yake pamoja na mengineyo tusiyoyajua.

Mkuu wa wilaya huyo wa Kisarawe akizungumza na Ayo TV amesema….”Kwanza nampongeza sana lakini nafikiri kwenye maisha yangu ni jambo la kihistoria kwasababu nimekuja kama mgeni mwalikwa lakini mmoja ya kati waliohitimu ni mchumba wangu”- DC Nikk wa Pili

“Mama Zuri mke wangu mtarajiwa ni mwanafunzi bora kuhitimu masomo ya CPA amepata zawadi ya shilingi Milioni 12 kiukweli ni kitu kikubwa kwetu”- DC Nikk wa Pili

“Amefanya mitihani wakati mtoto wetu alikuwa mdogo sana cha msingi ni kugawana malezi kwahiyo akienda kwenye masomo mimi nakaa na mtoto”- DC Nikki wa Pili

SIO MCHEZO..!! MCHUMBA WA NIKK WA PILI AVUNJA RECORD CHUONI KWAO ASHINDA MILIONI ZAIDI YA 12

Tupia Comments