Mix

Maneno ya Nikki wa II baada ya Rais Magufuli kuongea leo

on

Staa wa Bongofleva kutoka WEUSI Nikki wa Pili ameeleza na kumpongeza Rais Magufuli baada ya kuchukuwa uamuzi baada ya kupokea Ripoti ya Kamati Maalumu kuchunguza makontena ya Mchanga wa Madini yaliyozuiwa kusafirishwa nje ya Tanzania.

Nikki ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akimpongeza Rais kwa hatua hiyo ya kupambana na ufisadi akisisitiza kuwa vita ya kuvunja mfumo wa kifisadi ni hatari akitolea mifano ya sehemu mbalimbali viongozi walivyopotezwa pale walipojaribu kupambana juu ya haya.

>>>“Watanzania wanao pewa dhamana, wasipo amua kuwa waadilifu, umaskini uta andika historia tukufu kwa wa Tz, alafu kuha uhusiano gani kati ya uwekezaji na ufisadi…. maana kila kasha, wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara)…

“Yani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa nikwa makampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache…… nimpongeze mkuu wa nchi kwa kuamuwa kupambana na ufisadi huu…

“Ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari.. kina lumumba, nkruma, sankara, huko chile, nikaragwa, Venezuela, haiti, iran…. viongozi hawakupona….. ni vita kuu… Mungu akusimamie” – Nikki wa Pili.

Ikulu Rais Magufuli anakabidhiwa ripoti ya makontena, Wasanii waalikwa pia

Soma na hizi

Tupia Comments