Rapa na mwimbaji wa Nigeria, Chibuzor Nelson Azubuike, almaarufu Phyno, amesimulia jinsi alivyoshauriwa kujiunga na ibada au kufanya matambiko ikiwa alitaka umaarufu wa ghafla wakati wa siku zake kama msanii anayejitahidi.
Akiwa anaelezea kumbukumbu yake kwenye matukio mbalimbali ya muziki amewashauri wanamuziki wanaochipukia juu ya kuchukua njia za mkato kufikia mafanikio, Phyno alisema bidii, uamuzi na uthabiti vilimleta kufikia sasa.
“Kabla ya watu wengi kusikia kuhusu Phyno, nilikuwa na nyimbo ambazo hakuna mtu alijua zipo.
“Marafiki kadhaa waliniambia lazima nijiunge na ibada za giza au nitoe kitu au mtu fulani, nikawaambia bei ni kubwa sana. Sitafanya vile kamwe.
“Nilijiamini na nguvu ya kufanya kazi kwa bidii, nilianza kidogo na leo namshukuru Mungu,” alisema.
Phyno aliwashauri wasanii wachanga dhidi ya kukata tamaa, lakini wawe na moyo wa kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu.
Mwimbaji wa ‘Alobam’ aliwasihi “endeleeni kufanya kazi, muda ukifika, mtang’aa.”
Aliwaonya vijana wenye vipaji dhidi ya kukubali kurekodi mikataba bila kuzingatia masharti kwa sababu ya kukata tamaa, akisisitiza kwamba watajuta kwa muda mrefu.