Michezo

Nimekusogezea hapa matokeo ya Chelsea vs Wilsall na Liverpool vs Carlisle

on

Vigogo wengine wa England, vilabu vya Chelsea na Liverpool wakiwa kwenye viwanja tofauti nchini humo, leo walikuwa wakitafuta nafasi ya kucheza kwenye raundi ya kombe la Capital One.

  Chelsea wakiwa ugenini wamefanikiwa kuendelea kwenda raundi ya 4 ya michuano hiyo kwa ushindi 4-1 dhidi ya Wilsall.
  Magoli ya Chelsea yalifungwa na Ramires, Loic Remy, Kenedy na Pedro aliyefunga goli lake dakika za majeruhi.

Kwa upande mwingine, Liverpool walibidi kucheza kwa dakika 120 dhidi Carlisle ili kuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo –  baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1. Danny Ings akiwa mfunga upande wa Liverpool dakika ya 24 na Derek Asamoah akaisawazishia Carlisle dakika ya 35. Mechi imeamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Liverpool wamefanikiwa kushinda kwa penati 3-2.

Tupia Comments