Baada ya mchezo wa mchana kati ya Chelsea vs Everton, Barclays Premier League imeendelea kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti nchini Uingereza.
Arsenal wakiwa nyumbani waliikaribisha timu ngumu ya Stoke City- mechi ambayo imemalizika kwa vijana wa Arsene Wenger kupata ushindi wa 2-0.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Oliver Giroud.
Manchester City wakicheza ugenini leo wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao ya kushinda mechi zao zote za EPL kwa goli 1-0 dhidi ya Crystal Palace.