Michezo

Nimekusogezea matokeo ya Man U vs Burnley hapa

on

(null)
Baada ya kutoka sare ngumu dhidi ya wagonga nyundo wa London, Manchester United leo ilijitupa katika uwanja wake wa nyumbani kucheza na Burnley.

Mchezo huo ambao ulizaa kwa balaa baada ya United kumpoteza beki wake Phil Jones ambaye kutokana na majeruhi lakini dakika chache baadae walipata goli la kuongoza kupitia beki aliyembadili Chris Smilling.

Lakini dakika 3 katika dakika ya 11 ya mchezo Danny Ings aliisawazishia Burnley kwa goli safi la kichwa.

Sekunde kadhaa kabla ya mapumziko – Chris Smalling kwa mara ya pili akaipa United uongozi.
Kipindi cha pili Burnley walijaribu kusawazisha lakini juhudi zao hazikuzaa matunda baada Angel Di Maria kusababisha penati na Robin Van Persoe akaweka kambani goli la 3.

Kwa ushindi huo United wamepanda hadi nafasi ya 3 kwenye ligi wakiwa na pointi 47.

Tupia Comments