Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Nimekusogezea matokeo ya Simba vs Azam FC hapa

on

  

Wiki moja baada ya klabu ya Dar Young African kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom, vita sasa imehamia katika kugombea nafasi ya pili katika ligi hiyo kati ya Simba na Azam.

Vilabu hivyo viwili vya jijini Dar Es Salaam, leo vilikutana katika dimba la uwanja wa taifa.

Mchezo huo uliomalizika hivi punde umeisha kwa Simba kutoka kifua mbele kwa kupata ushindi wa magoli 2-1.

Simba ndio ilianza kufunga goli katika dakika ya 48, kupitia kiungo hatari Ibrahim Ajjib, lakini muda mfupi baadae akitokea benchi kiungo Mudathiri Yahaya akaisawazishia Azam.

Dakika ya 74, mshambuliaji Ramadhan Singano ‘Messi’ alikata mzizi wa fitna na kuifungia Simba goli la pili na la ushindi, na mpaka mwamuzi anapuliza kipenga ubao wa matokeo ulikuwa unaonyesha – Simba 2-1 Azam FC.

Tupia Comments