Michezo

“Nimemsikia msemaji wao kasema maneno ya ovyo, Ubingwa wetu wa kupewa”-Manara

on

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara leo amewasili jijini Dar es Salaam akitokea Mbeya na kikosi cha Simba SC walipokuwa wakicheza mechi zao za Ligi Kuu, Manara ameeleza kuwa sababu ya kuwasili kimya kimya ni kutotaka kufanaya sherehe za Ubingwa hadi wacheze mechi yao ya robo fainali ya FA dhidi ya Azam FC.

“Tutawatangazia ratiba inayokuja kwa sasa tunaangalia mchezo wa FA dhidi ya Azam FC lakini kwanza kipaumbele ni mechi dhidi ya Azam, tunaenda kucheza na timu ambayo tunaiheshimu sana ina ubora mkubwa sana ina uwezo mkubwa sana”>>> Haji Manara

“Nimesikia msemaji wao ameniponda nimesikia amesema sisi wachezaji wetu Ubingwa wetu wa ovyo Ubingwa wa kupewa ni lugha ambazo hazipaswi kuongelewa katika mpira wa sasa sisi tunaiheshimu Azam wala hatusemi timu ya ovyo wala hatusemi chochoe kibaya kuhusu Azam”>>> Haji Manara

vbbb

Soma na hizi

Tupia Comments