Gabriel Jesus yuko njiani kupata nafuu baada ya kupata jeraha la gotu mapema mwezi huu.
Mshambuliaji huyo wa Brazil alichapisha update ya jeraha lake kupitia Instagram mapema Jumatano baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake.
“Siku zote kutakuwa na majibu kwa kila kitu, ambayo tutajua tu baadaye. Ninaamini na kumtumaini Mungu,” mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliandika huku akishiriki picha yake akitabasamu na magongo mikononi mwake.
Jesus, ambaye alipata jeraha katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United, atakosa msimu uliosalia akiwa na Arsenal.
Ni mara yake ya pili kukumbwa na hali mbaya kama hii kwani alikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2022/23 kutokana na jeraha tofauti la goti.
Jesus ni mmojawapo wa nyongeza za hivi punde kwenye orodha ndefu ya majeruhi ya Gunners pamoja na White, Tomiyasu, Saka na hivi majuzi Saliba, na kumfanya Mikel Arteta kutafuta nyongeza katika dirisha la uhamisho la Januari.
“Tunatafuta soko kwa bidii ili kuboresha kikosi,” Mhispania huyo alithibitisha wiki iliyopita.