Mchezaji Nyota wa Paris St-Germain ya Ufaransa Neymar da Silva Santos Junior raia wa Brazil 🇧🇷 jana alisaini mkataba wake mpya kuendelea kuitumikia PSG hadi 30 Juni 2025.
“Nimefurahia sana kuendelea na safari yangu hapa Paris Saint-Germain” amesema Neymar Jr wakati wa kusaini mkataba wake mpya.
“Nina furaha sana hapa Paris, na ninajivunia kuwa sehemu ya kikosi hiki, kufanya kazi na wachezaji hawa, kocha mzuri na kuwa sehemu ya historia ya klabu hii. Haya ni mambo ambayo yananifanya niamini hata zaidi katika mradi huu mzuri. Nimekua kama mtu hapa, kama mwanadamu na kama mchezaji, pia. Kwa hivyo ninafurahi sana kuongeza kandarasi yangu na ninatarajia kushinda makombe mengi hapa “ Neymar