Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amempongeza Waziri wa Maji Jumaa Aweso, kwa kuchukua maamuzi ya kuwafukuza wakandarasi feki wa mradi wa maji uliopo Mwanga na kumweleza kuwa kama angechelewa basi angemfukuza yeye.
“Watanzania wamechoka kusubiri miradi, nataka miradi ikamilike mapema na isiwe inazaa variation, nimeshukuru umeanza kuchukua hatua kwa wakandarasi feki waliokuwa kule Mwanga ukawafukuza kwa sababu ungechelewa kuwafukuza mimi ningekufukuza wewe ni vizuri wale wanaokuchelewesha wewe fukuza tu” Rais Dkt. Magufuli.
“Pia wale wakandarasi uliowafukuza, zungumza na bodi ya wakandarasi wafutwe na wasipate kazi yoyote Tanzania kwa vile tuna ushirikiano wa Nchi za Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki peleka majina yao kule hatuhitaji wakandarasi matapeli, Waziri umeanza vizuri na moto ulioanza nao endelea nao, usicheke na hawa wakandarasi cheka na maji unapokuwa unayanywa” Rais Magufuli