AyoTV

Mwigizaji Nisha yuko China kwa mara yake ya 7.. watu wanamuhisi vingine ila kaongea yafuatayo

on

Mwigizaji wa bongomovie Salma JabuNisha’ amekwenda tena China ikiwa ni mara yake ya saba toka aanze kwenda China ambapo wengi wa mashabiki zake wamekua wakihisi anafanya biashara haramu ya dawa za kulevya kama wanavyotumika baadhi ya Wasichana wa Kitanzania.

Mtangazaji Millard Ayo alimpata Nisha kwa simu na Interview yake kusikika kwenye AMPLIFAYA CloudsFM March 16 2016 na kusema haya >>> ‘Hii ni mara yangu ya saba kwa kipindi cha miaka miwili, tofauti na usanii mimi ni Mfanyabiashara nauza nguo, viatu, nywele na dawa za kupungua na nikirudi nawafungulia duka la Harusi na duka la Birthday

Nilishawahi kuripotiwa kukamatwa na dawa za kulevya China lakini haikuwa kweli, nimeshapata maswali na maneno sana kwamba nasafirisha dawa za kulevya ila sio kweli… mimi popote ambapo riziki ipo nakwenda, sasa hivi pia naanza kusomea biashara China, Ujasiriamali kwa muda wa miezi mitatu…. nitakua narudi TZ kila wiki sababu ya kusimamia biashara zangu’ – Nisha

Ukihitaji kumsikia Nisha mwenyewe unaweza kubonyeza play kwenye hii audio hapa chini…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments