Top Stories

Mtanzania alietengeneza Gari linalotumia Umeme “halina Injini na hatuendi Sheli” (+video)

on

Wakati kwenye Nchi kama Marekani tayari magari yanayotumia umeme yanayotengenezwa na Kampuni ya Tesla yameshaanza kutumika barabarani huku moja ya aina za magari hayo ikigharimu zaidi ya MILIONI 80, hapa Tanzania kuna Mtanzania Gabriel Jeremia na yeye katengeneza Gari lisilotumia mafuta bali umeme.

Gabriel anasema “Binafsi nilikua na idea ya kutengeneza gari ambalo linaweza kutumia mfumo wa umeme kujiendesha, niliiweka ile idea kwenye maandishi, hii gari hapo mbele haina injini kama gari za kawaida bali inatumia umeme wa betri na kuna mota ipo kwenye matairi ya nyuma, kinachofanyika hapa tuna-control umeme wa betri kwenye magurudumu ya nyuma, tukipeleka mwingi basi gari itakimbia zaidi, na ina uwezo wa kutembea umbali wa kilometa 90 betri ikiwa imejaa

Pia utakapochaji utachaji kwa kiwango cha umeme cha uniti tatu umeme wa majumbani kama unavyochaji simu, inagharimu kama shilingi elfu moja na mia mbili kwa pesa za Tanzania ambapo kwa hiyo shilingi 1200 unaweza kuchaji hili gari na kutembea nalo kwa umbali wa kilometa 90bonyeza play hapa chini kumtazama mwanzo mwisho

VIDEO ILIYONASA WEZI BILA KUJUA KWAMBA WANAREKODIWA WAKIIBA OFISINI DAR ES SALAAM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

MAZOEZI YA KIJESHI CHINA “KATA KONA BILA USUKANI” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments