Top Stories

“Nitafoka kwa kalamu, Waziri sio mpiga mizinga” Rais Samia (+video)

on

“Nimeamua kuvunja taboo ya muda mrefu kwamba Wizara ya Ulinzi lazima akae Mwanaume mwenye misuli yake lakini kazi ya Waziri kwenye Wizara ile sio kupiga mizinga wala kubeba bunduki ni kusimamia sera na utawala wa Wizara, nikaamua Dada yetu Dr. Tax nimpeleke huko”

“Kipindi chote tukienda SADC, Dr. Tax alikuwa anasimamia vizuri mambo yote ya usalama ndani ya region na alikuwa ana upeo mkubwa katika maeneo ya Afrika Mashariki kwahiyo kwa uzoefu alioupata katika masuala ya usalama anakwenda kutusaidia huko, yeye anajua vizuri Askari wetu waliopo Msumbiji, DRC Congo na kwanini wapo huko mifumo yao, wanavyobadiliia na pia haki zao”————Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi wapya leo Ikulu, Dodoma

“Mawaziri wapya natumaini mtakwenda kufanya vizuri, uteuzi wenu hauna maana nyie ni wazuri kuliko waliokuwepo uzuri wenu utaonekana katika kazi, hata tuliowateua mwanzo walikuwa wazuri, nataka kuona matokeo sitaki kuwaona kwenye TV tu mnafanya hili mnafanya lile”

“Katika kipindi cha miezi sita ya Urais wangu nilijaribu kuwa mkimya na utulivu na nikawa nasoma Wizara zote yapo mengi ya kurekebisha, wapo pia ambao wakati nawasoma nao wakanisoma, wapo waliochukulia ukimya wangu na utulivu wangu kama udhaifu na wengine wakafanya kazi nzuri”

“Kipindi cha miezi sita ya Urais wangu nilikuwa najifunza, katika Uongozi kuna mbinu nyingi, Serikali yetu itaendeshwa na matendo makali na sio maneno makali, matendo makali sio kupigana mikwaju ni kwenda kwa Wananchi kutoa huduma inayotakiwa kila Mtu kufanya wajibu wake”

“Msitegemee kwa maumbile yangu haya pengine na malezi yangu kukaa hapa nianze kufoka nahisi sio heshima, na kwasababu nafanya kazi na Watu wazima naamini wanajua wanachokifanya, sitokaa nikaanza kufoka kwa maneno, nitafoka kwa kalamu” ———-Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi wapya, Ikulu Dodoma leo

Soma na hizi

Tupia Comments