Kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayekipiga katika klabu ya Dar Es Salaam Young African Haruna Niyonzima October 15 amefunga ndoa na mzazi mwenzake. Haruna Niyonzima ambaye alifunga ndoa hiyo baada ya kurejea kutoka Rabat Morocco mji ambao walienda kucheza mechi na timu ya taifa ya nchi hiyo.
Niyonzima ni baba wa watoto wa tatu mmoja wa kiume na wawili ambao ni mapacha Atifa na Atika. Niyonzima na mkewe walifunga ndoa ya kiserikali Kigali Rwanda. Hata hivyo kufuatia kuchelewa kujiunga na kambi ya klabu yake ambayo Bagamoyo ya kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC, huenda Niyonzima akakosa mchezo huo.
Chanzo cha picha hizi ni: izubarirashe.rw
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.