Michezo

Taarifa kuhusu kuugua kwa Haruna Niyonzima akiwa Misri

on

MMG25771Mchezaji tegemezi wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima ameugua ghafla akiwa huko jijini Alexandria Misri wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly utakaopigwa muda mchache kutoka sasa.

Niyonzima ambaye aliondoka akiwa na afya njema alianza kuugua malaria jana usiku na leo asubuhi ikaonekana hatoweza kuitumikia Yanga katika mechi hiyo ambayo inatakiwa kuulinda ushindi wake wa bao moja iliyopata wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mchezo huo endelea kutembelea millardayo.com

Tupia Comments