AyoTV

VideoFUPI: Mazingira ya Yusuph Manji kuchukuliwa na gari la Wagonjwa Polisi

on

Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji amekua akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.

Jioni ya leo February 12 2017 Mfanyabiashara huyo amechukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na haijajulikana limempeleka wapi lakini alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.

Polisi hawakuruhusu Waandishi wa habari karibu na eneo hilo lakini hii hapa chini ni video fupi ya mazingira ya Yusuph Manji kuondolewa kwenye eneo hilo.

VIDEO: Alichozungumza Yusuph Manji baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu 65 ya Paul Makonda kwenye sakata la dawa za kulevya

VIDEO: “Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5 wewe ni nani? – MBOWE……. Full video hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments